CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE
KITIVO CHA KILIMO
IDARA YA SAYANSI YA CHAKULA NA TEKNOLOJIA
TAARIFA YA TUME TEULE YA WANAFUNZI WA SHAHADA YA SAYANSI YA CHAKULA NA TEKNOLOJIA JUU YA UWEPO NA UTENDAJI KAZI WA TAFOST NCHINI
IMEANDALIWA TAREHE 1O MAY, 2011.
IFUATAYO NI TAARIFA YA KIKAO KATI YA WAJUMBE WANAFUNZI KUTOKA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE SHAHADA YA SAYANSI YA CHAKULA NA TEKNOLOJIA NA VIONGOZI WA TAFOST.
UTANGULIZI.
Kikao kilianza mnamo saa tano asubuhi, kikiwa kime hudhuriwa na wajumbe Tisa na kufunguliwa na mwenyekiti wa TAFOST, Kiki fuatiwa na utambulisho wa wajumbe kama ifuatavyo:-
MWENYEKITI WA TAFOST MR. G. CHIPONGO.
KATIBU WA TAFOST DR. R. WIGENGE.
MJUMBE WA KAMATI KUU YA TAFOST DR. M.KIMANYA.
MWENYE KITI WA WAJUMBE ESTON YESAYA.
KATIBU WA WAJUMBE KIGAVA ANYOMBYE.
MTUNZA HAZINA WA WAJUMBE MUSHENGEZI PERPETUA.
MJUMBE RUGEMALIA KELVIN.
MJUMBE MWINYALA JOHN.
MJUMBE MBAJIJE BARAKA.
HISTORIA YA TAFOST.
Wahitimu wa kwanza wa sayansi ya chakula na teknolojia wapatao 12 mnamo mwaka 1989. Walishauriwa na wahadhili Professor Maeda, Laswai na Tiisekwa kuwa waende wakaitangaze vema shahada ya sayansi ya chakula na teknolojia, nanukuu “GO AND SHOW THE WORLD THAT WE ARE EXISTING”. Ndipo wahitimu hawa wakapata wazo la kuanzisha chama kitaka cho waunganisha wafanyakazi na wanafunzi wa sayansi ya chakula na teknolojia.
Wahitimu hawa walitamani chama hicho kianzishwe chuoni Sokoine. Lakini Wahadhili waka washauri waanzishe chama hicho nje ya chuo ili kiwa nufaishe wanachama na kisionekane kuwa ni chama cha kitaaluma zaidi.
Wakiwa nje ya chuo wakaanza mchakato wa kuunda katiba ya chama hicho wakizingatia miundo ya vyama vingine Kama vile chama cha sayansi ya chakula na teknolojia cha Uingereza na chama cha sayansi ya chakula na tekinolojia cha Marekani. Katiba ilipo kamilika, walisajili chama Kwa kutumia pesa zao wenyewe mnamo mwaka 1993 na hii ilikuwa baada ya kuridhiwa na wizara tatu ambazo ni Wizara ya kilimo na chakula, Wizara ya viwanda na biashara na Wizara ya Afya. Toka kusajiliwa uongozi ulikuwa chini ya Mwenyekiti GAUDENCE CHIPONGO na Katibu RAYMOUND WIGENGE. Ambao ni viongozi mpaka sasa. Chama hiki kime endelea kuongozwa na pesa za kujitolea kutoka kwa viongozi na wajumbe na kila mwanachama alipaswa kuchangia kiasi kisicho pungua Tsh 10,000/= na kufanikiwa kufungua akaunti katika benki ya NMB. Hakukuwa na ofisi maalumu kutokana na viongozi kubanwa na majukumu mengine ya kiserekari.
Mnamo mwaka 2005 walipata ofisi katika jengo la NSSF Ubungo maziwa. Hata hivyo ofisi hiyo haikudumu kutokana na kukosekana kwa pesa za uendeshaji hivyo ilifungwa mapema mwaka 2006 ikiwa na deni la pango la nyumba kiasi cha Tsh 600,000 na kukiacha chama bila ofisi mpaka leo. Hata hivyo wanachama waliendelea kukutana eneo la river side kwakuwa kilikuwa kituo cha kati baina Yao, wakijadili jinsi ya kukiendesha chama ambacho Kwa sasa kipo katika “LATENT STAGE” Kama mwenyekiti alivokiita.
Kwasasa chama kina wanachama wapatao 50, wanao patikana maeneo mbalimbali kama vile TBL, TFDA, BAKHRESA, PEPSI na Kwa MKEMIA MKUU WA SERIKALI.
MAFANIKIO.
Yafuatayo ni mafanikio yaliyopatikana toka kuanzishwa kwa TAFOST.
(i) Kusajili chama serikarini.
(ii) Kufungua akaunti ya chama.
(iii) Kuongezeka idadi ya wanachama Toka 12 hadi 50.
(iv) Chama kime saidia sayansi ya chakula na technolojia kutambulika serikarini katika wizara zifuatazo:-
Ø Wizara ya Afya,
Ø Wizara ya Viwanda na biashara na
Ø Wizara ya kilimo na chakula.
(v) Kuwa na mawasiliano na vyama vya sayansi ya chakula na tekinolojia nchini Marekani na Uingereza.
(vi) Kuanzisha jitihada ya kuanzishwa kwa “scheme of service” ya sayansi ya chakula na tekinolojiana na kugundua kuwa wataalamu wa sayansi ya chakula na tekinolojia wanatambuliwa kama wakemia katika wizara ya afya.
(vii) Viongozi wametumia nafasi walizo nazo, mfano katibu wa chama na wajumbe kutoka, TFDA idara ya chakula wamehimiza kila kiwanda kuwa na mtaalamu wa sayansi ya chakula na tekinolojia na hili limefanikiwa.
(viii) Kuhimiza kazi za utaalamu wa chakula zifanywe na wataalamu wa chakula.
CHANGAMOTO.
Richa ya mafanikio yalio elezwa hapo juu. TAFOST ina kabiliana na changa moto mbalimbali kama ifuatavyo:-
(i) Ukosefu wa pesa Kwa ajili ya kuendesha shughuli za chama.
(ii) Mwamko mdogo miongoni mwa wanachama.
(iii) Mawasiliano hafifu baina ya wanachama.
(iv) Kukosekana kwa mtu asiye na majukumu mengine ya kiofisi ili kuendesha shughuli za chama ofisini.
(v) Idadi ndogo ya wanachama.
(vi) Akaunti imesitishwa kutokana na kuto tumiwa kwa mda mrefu.
(vii) Chama kime sitishwa kutokana na kukosa pesa ya kulipa serikalini.
(viii) Kupoteza nafasi mbalimbali mfano kutokana na kukosa pesa ya kulipia bandarini journals za sayansi ya chakula zilishindwa kuingazwa nchini.
MAAZIMIO.
1. Kufufua akaunti ya chama Kwa kujichangisha pesa wanachama wanafunzi na waajiliwa.
2. Kutolewa kwa cheti kwa wana chama wanafunzi wanao hitimu sayansi ya chakula na teknolojia.
3. Kurekebishwa Kwa katiba ya chama kwani haiendani na wakati kwa baadhi ya vipengele.
4. Kuanzishwa kwa uongozi mdogo vyuoni Kama matawi ya TAFOST.
5. Chama kiwe na mfumo wa mawasiliano Kama mail address na web.
6. Kutakuwa na kikao cha wanachama wa TAFOST mwezi wa nane, ambapo uchaguzi mkuu Utafanyika sikuhiyo.
7. Wanafunzi na wanataaluma walio ajiliwa wajadiliane kilamtu achangie kiasi gani na mwisho wa michango iwe ni mwezi wa sita, ili kusaidia kufufua chama serikalini na mwanzo wa mfuko kwa chama.
HITIMISHO.
Ndugu wajumbe kwa kuzingatia uhalisia wa chama, kuna umuhimu mkubwa wakuunganisha jitihada za sisi kama wanafunzi na wanachama wote wa TAFOST kufufua na kuimarisha chama ili kiweze kutetea maslahi yetu kama wanachama wa talaamu wa sayansi ya chakula na technolojia kitaifa.
Kwa niaba ya kamati teule, napenda kutoa shukrani za dhati kwa uongozi wa TAFOST kwa ushirikino mkubwa walio uonesha kwa kamati. Shukrani za pekee ziufikie Ungozi wetu chini ya Mwenyekiti Oraph Mhema na katibu Minja Eliaka pamoja na jopo lao kwa ushirikiano walio uonesha kwa kamati hii teule, wakati wote tulipo hitaji msaada wao. Mwisho kabisa shukrani zetu ziwafikie viongozi wote wa madarasa na wanafunzi kwa ujumla wao kwa ushirikiano wenu mkubwa na kamati hii na ni matarajio ya kamati kuwa ushirikiano huu utadumishwa kwa manufaa yetu sote.
AHSANTENI KWA KUSIKILIZA.
No comments:
Post a Comment