Tanzania
Institute of food Science and technology ni taasisi ambayo imeundwa kutoka
kwenye chama kilichokuwa kikiitwa Tanzania association of food scientists and
technologists ambacho kiliundwa mnamo mwaka 1993. TIFST imeanzindiliwa rasmi
tarehe 13th April 2012 na Mheshimiwa katibu wa wizara ya viwanda na
biashara Bi Joyce Mapunjo, Ikijumuisha wajumbe mbalimbali kutoka mashirika ya
umma na yale ya binafsi kama vile TFDA, TBS, ASAS na SIDO na wanafunzi kutoka chuo kikuu cha kilimo cha
sokoine
Tanzania
Institute of food science and technology imeanzishwa baada ya kuona kuwa Tanzania association of
food scientists and technologists ni ya kitaaluma zaidi na ilikuwa haihusishi watu mbalimbali ambao
walikuwa wakijihusisha na masuala mbalimbali ya chakula kama vile wasindikaji
wadogo wadogo wa vyakula
Mawazo
ya kukianzisha chama hiki cha Tanzania Institute of Food Science and Technology
yalianzishwa na DR Anne Perrera ambaye ni mwenyeji wa New Zealand kupitia New
Zealand Institute of Food Science and Technology baada ya kufika Tanzania kama
mtu wa kujitolea katika fani ya lishe na chakula SIDO Arusha. Baada ya kuwa
amefika Tanzania DR Anne akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Rose Maeda walifika
mpaka Wizara ya mambo ya ndani kuangalia kama kuna chama chochote kile ambacho
kimekwisha sajiliwa hapo ofisini ambacho kinajuhusisha na maswala ya chakula,
ndipo walipoambiwa habari ya TAFST.
Baada ya maelezo ya kina kutoka ofisi ya msajili wa vyama walibaina kuwa baadhi
ya viongozi wa TAFST wapo TFDA na ndipo walipofunga safari mpaka ofisi y a TFDA
Kwa Wegenge ili kupata maelezo zaidi. Baada ya kupata maelezo ya kina kutoka
kwa Wegenge pamoja na ofisi ya msajili wa vyama waligundua kuwa chama kilikuwa
hakiko hai na baada ya kupitia pia katiba yake waligundua kuwa chama hicho
yaani TAFST kilikuwa na mapungufu mengi kama vile chama kilikuwa cha kitaluma
zaidi na kilikuwa hakiwapi nafasi watu ambao sio wanataaluma wa Sayansi ya
chakula na Technologia. Hivyo DR Anne pamoja na Rose Maeda waliuamua kuanzisha
mchakato wa kuanzisha chama kipya ambacho kitawajumisha wanataaluma ya sayansi
ya chakula na technologia pamoja na wadau mbalimbali wanaojuhusisha na masuala
ya chakula kama vile wasindikaji wadogo wadogo wa vyakula pamoja na kampuni
kubwa kubwa ambazo zinajihusisha na masuala pia ya chakula. Waliamua
kuwasiliana na wadau wachache wanajihusisha na masuala ya chakula kama vile
Wahadhili kutoka chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine idara ya chakula ambao ni
Prof Tiisekwa, Prof Chove na Prof Laswai pamoja na wadau wengine ambao
wameainishwa kwenye katiba. Wadau hawa waliamua kuipitia katiba ya TAFST kwa
kina na kubaina mapungufu ambayo yalipelekea wote kwa pamoja kupendekeza na
kuamua kuanzishwa kwa Tanzania Institute of Food Science and Technology kwa
kutumia malekebisho ya katiba ya TAFST ikiwa ni pamoja na kuzingatia mifumo ya
vyama kama hivyo Duniani
Mpaka
sasa chama kimeshasajiliwa kwa msajili wa vyama ( MINISTRY OF HOME AFFAIRS) na
hakina ofisi lakini kwa sasa wanatumia ofisi za TPSF ambazo ziko Msasani chini
ya viongozi wafuatao, m/kiti ni Neema D. Mrema ambaye ni Food technology
specialists, na katibu wake ni Rose
Maeda ambaye ni Cluster development specialist.
Chama
kitakuwa chini ya usimamizi wa wizara ya viwanda na biashara ingawa mapendekezo
yao ya awali ilikuwa chama kiwe chini ya ofisi ya waziri mkuu. Utaratibu wa
kutafuta sehemu ya ofisi wizara husika inashughulikia
Wadau
ambao walihudhulia kikao ambacho kilifanyika Ubungo plaza walipata fulsa ya
kuisoma katiba vizuri na kutoa mapendekezo yao ikiwamo suala la wanafunzi
kuingia katika Board of Directors wote kulikubali suala hili. Baada ya
mapendekezo na malekebisho mbalimbali kutoka kwa wadau katiba ilipitishwa na
ndiyo sasa katiba ambayo inatumika sasa
Chama
kwa sasa kiko kwenye michakato ifuatayo; kujiunga na chama cha sayansi ya chakula na
technolojia cha dunia (IUFOST), Usajili wa wanachama katika ngazi tofauti
tofauti kama vile zilivyoainishwa kwenye katiba, upatikanaji wa nembo ya chama
, kuongeza na kuanzisha vyanzo vya mapato kwa ajili ya shughuli mbalimbali za
chama na upangaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya chama.
Chama
kitakuwa na aina kuu tano za uanachama kama vile zilivyo ainishwa kwenye katiba
na kutakuwa na ada ya uanachama kutokana
na ngazi au aina ya uanachama ambao utakuwa nao, na kila mwanachama atatakiwa
kujaza fomu za uanachama ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli zote za chama .Imeandaliwa
na;
Katibu
Elson
Backila (0712 733685)

No comments:
Post a Comment